Mamilioni ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya Iran na baadhi ya nchi nyingine walijitokeza kushiriki katika mazishi ya Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, wakionesha heshima, mapenzi na mshikamano wao kwa Kiongozi huyo.

6 Julai 2026 - 23:28

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Mamilioni ya waombolezaji walifurika katika barabara na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (Allah Amrehemu), nchini Iran.

Umati mkubwa wa wananchi kutoka mikoa mbalimbali ya Iran pamoja na wageni kutoka nje ya nchi ulijitokeza kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo, huku barabara na viwanja vikijaa waombolezaji waliokuwa wakionesha hisia za huzuni, mapenzi na mshikamano.

Maelfu na Mamilioni ya Waombolezaji Washiriki Katika Mazishi ya Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei nchini Iran+Picha

Mahudhurio hayo makubwa yameelezwa na waangalizi na wafuasi wake kuwa ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa iliyowahi kushuhudiwa katika mazishi ya kiongozi wa kisiasa na kidini nchini Iran, yakidhihirisha nafasi aliyokuwa nayo Ayatollah Sayyid Ali Khamenei katika nyoyo za wafuasi wake na sehemu mbalimbali za ulimwengu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha